1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Jeshi la Urusi laingia katika mkoa wa Kharkiv nchini Ukraine

10 Mei 2024

Urusi imefanya mashambulizi ya kuvuka mpaka kuelekea mji wa Kaskazini Mashariki mwa Ukraine wa Kharkiv, kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya ulinzi ya Ukraine na chanzo kimoja cha kijeshi.

https://p.dw.com/p/4fiig
Mapamano katika mkoa wa Kharkiv
Kumetokea milipuko katika maeneo ya makaazi jimboni Kharkiv baada ya Urusi kuingia eneo hiloPicha: Anadolu/picture alliance

Taarifa ya wizara imedai kuzuia mashambulizi hayo lakini mapigano makali bado yanaendelea na kwamba Urusi imeanzisha mashambulizi ya angani karibu na eneo la mpaka.

Soma pia: Wanne wajeruhiwa kwa shambulizi Urusi katika mkoa wa Kharkiv

Chanzo kingine cha ngazi ya juu ndani ya jeshi la Ukraine kilisema Urusi ilipiga hatua kadhaa umbali wa "kilometa moja" kuelekea Ukraine na inajaribu kuzuia mashambulizi ndani ya eneo la Urusi.

Ukraine ilifanikiwa kuvirejesha nyuma vikosi vya Urusi kutoka eneo kubwa la Kharkiv mwishoni mwa 2022, lakini mashambulizi ya Moscow sasa yamepamba moto, mnamo wakati vikosi vya Kyiv vikikabiliwa na uhaba wa silaha.